UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (Ovarian Cyst) Habari za mda huu ndugu wapenzi na karibuni katika wasaa mwingine, Leo tutajadili kuhusu uvimbe katika mayai ya mwanamke au kwa maneno mengine ovarian cyst, Karibuni kama utakuwa na swali lolote unakaribishwa pia. Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu kwa sasa kutokana Na mifumo ya maisha Na ulaji umekuwa ukiwatokea wanawake wa umri wowote ule ingawa kwa kipindi cha nyuma mara nyingi ulikuwa ukionekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. Lakini kwanza hebu tufahamu juu ya mayai ya mwanamke. Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa u...